Mwaka 2023, ushirikiano wa kirafiki na wa kunufaishana kati ya China na Russia umekuwa na matokeo yenye manufaa. Chini ya mwongozo wa kimkakati wa wakuu hao wa nchi, mabadilishano ya kiuchumi na kibiashara baina ya nchi hizo mbili yamefikia ushirikiano mpya wa hali ya juu na wa kivitendo katika nyanja mbalimbali. Kuanzia mwaka 2024 hadi 2025, kwa kuadhimishwa kwa Mwaka wa Utamaduni wa China na Urusi, mawasiliano kati ya watu na watu kati ya nchi hizo mbili yataongezeka zaidi, na kuweka uungaji mkono thabiti wa umma kwa uhusiano wa pande hizo mbili.